Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ilianza ujenzi wa jengo la ofisi ya makao makuu ya Wilaya mwaka 2011/2012. Lengo lilikuwa ni kujenga jengo la ghorofa 4, lakini katika mwaka 2013/2014 Halmashauri iliamua kupunguza ghorofa kutoka 4 hadi ghorofa 2. Ujenzi umefanyika katika awamu III, awamu ya I ilianza tarehe 22/09/2011 na ilihusisha kazi za ujenzi wa msingi, kumwaga jamvi la sakafu ya chini na kuinua nguzo za wima zitakazopokea sakafu ya kwanza. Mkataba awamu ya I uligharimu Shilingi 709,856,492.00 na kazi za awamu ya I zimekamilika zote.
Awamu ya II ya ujenzi ilianza tarehe 06/07/2012 na ujenzi ulihusisha kazi za ujenzi wa sakafu ya ghorofa ya I na ujenzi wa nguzo za wima za kupokea ghorofa ya pili. Shughuli hizi zimegharimu jumla ya Shilingi 717,627,455.00 na ujenzi awamu ya pili umekamilika.
Ujenzi awamu ya III unahusisha kazi ya ujenzi wa sakafu ya pili na nguzo zitakazo pokea lenta. Hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa Shilingi 383,911,780.10 ambapo gharama ya mkataba ni Shilingi 626,571,036.72. Kazi haijakamilika na ujenzi unaendelea.
Kazi za ujenzi awamu zote III zimetekelezwa na Mkandarasi Brave Engineering and Construction Company Limited na jumla ya fedha zilizotumika katika awamu zote III ni Shilingi 1,811,395,727.10.
Aidha ujenzi unasimamiwa na Mhandisi Mshauri Mekon Arch Consult. Jumla ya gharama za Mkataba ni Shilingi 142,050,000. Kazi za Mhandisi Mshauri zinahusisha usanifu wa michoro kuandaa BOQ na kufanya usimamizi wa ujenzi.
Ujenzi ulipofikia na kukamilika unakisiwa kugharimu Shilingi 4,369,851,448.14 hadi kukamilika.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa