AFYA TIBA
Idara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa afya wa mwaka 2015 -2020. Katika kuhakikisha wananchi wanapata tiba sahihi, idara imekuwa ikitekeleza majukumu yafuatayo:
i.Kusimamia manunuzi ya dawa, vitendanishi vya maaabara ,vifaa na vifaa tiba kisha kuvisambaza kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
ii.Kutoa huduma za matibabu na uuguzi kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya zikiwemo huduma za upasuaji mkubwa na mdogo. Huduma hizi ni kwa wagonjwa wa nje na wagonjwa wa kulazwa.
iii.Kufanya ukaguzi wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
iv.Kusajili na kuhuisha maduka ya dawa na vipodozi, kuyafanyia ukaguzi mara kwa mara na kuhakikisha yanafuata sheria, kanuni na miongozo inayosimamia uanzishaji na uwepo wa maduka hayo
v.Kusimamia pamoja na kuzikagua maabara zote na kuhakikisha zimesajiliwa na zinatoa huduma bora kulingana na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya.
vi.Kutoa, kusimamia na kuratibu huduma za afya ya uzazi na mtoto katika Manispaa . Huduma hizi ni pamoja na uzazi salama, huduma za uzazi wa mpango, huduma za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito, uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti. Huduma nyinginezo ni pamoja na huduma za kuzuia ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.
vii.Kuratibu huduma za kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI. Huduma zitolewazo ni pamoja na matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, huduma za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto, huduma za kuchunguza na kutibu magonjwa ya ngono pamoja na huduma za wagonjwa majumbani. Huduma hizi hutolewa katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
viii.Idara inashughulikia pia masuala ya ustawi wa jamii ambapo inahakikisha makundi maalumu yanaatambuliwa na kuunganishwa na mpango wa matibabu bila maalipo. Makundi haya ni pamoja na wazee, walemavu na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
AFYA KINGA
Idara imeendelea kutekeleza majukumu mbalimbali yanayolenga kuwakinga wananchi na magonjwa ya kuambukiza. Mojukumu hayo ni pamoja na:
i.Ukaguzi wa nyumba za kuishi na majengo ya biashara kama vile nyumba za kulala wageni,majengo ya kutengeneza na kuuza vyakula ili kuondoa machukizo yanayoweza kuhatarisha afya ya binadamu.
ii. Utoaji wa elimu ya afya kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya afya.
iii.Utoaji wa chanjo kwa magonjwa ya kuambukiza kwa wajawazito na watoto
iv.Usimamizi wa afya na usalama mahala pa kazi
v.Usimamizi wa usafi wa Mazingira.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa