Utangulizi
Jina la Mkuu wa Idara: Tito Elias Luchagula
Namba ya simu: 0745 517798
Email: luchagula.titus@gmail.com
dcdo@sikongedc.go.tz
Idara ya Maendeleo ya Jamii inajumla ya watumishi 13 Mahitaji ni 27 na upungufu ni watumishi 14.
Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Jamii
Takwimu muhimu za Idara
i)Idadi ya vikundi na kiasi cha mkopo kilichotolewa
Sn
|
Mwaka
|
Idadi ya vikundi
|
Kiasi kwa mwaka
|
1
|
2014/2015
|
12
|
8000,000/=
|
2
|
2015/2016
|
36
|
33,500,000/=
|
3
|
2016/2017
|
119
|
121,000,000/=
|
4
|
2017/2018
|
104
|
138,000,000/=
|
ii)Idadi ya Asasi Zisizo za Kiserikali:
IDADI
|
|||
NGO’s
|
CBO’s
|
FBO’s
|
JUMLA
|
3
|
48
|
2
|
53
|
iii) Maambukizi ya virusi ya Ukimwi
Mwaka
|
Idadi ya waliopima
|
Waliokutwa na maambukizi
|
Asilimia
|
2015
|
19,939
|
843
|
4.2
|
2016
|
33,603
|
1057
|
3.1
|
Hadi Juni 2017
|
18,237
|
493
|
2.7
|
Mafanikio
Elimu ya ujasiriamali ilitolewa kwa wanawake na Vijana wapatao 835 Mwaka 2014 hadi 2017
Kutolewa kwa mikopo yenye riba nafuu kwa vikundi vya ujasiliamali vya wanawake na Vijana.
Kuongezeka kwa vikundi vya Vikoba kutoka 34 hadi Kufikia vikundi 90 kutoka mwaka 2014 hadi 2017
Jamii kupata uelewa juu ya Ukweli kuhusu ukimwi na hivyo kujitokeza kupima afya kwa hiari
Changamoto:
Upungufu wa wataalamu wa Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Kata na Vijiji.
Uhaba wa vitendea kazi kama usafiri, Ofisi na samani.
Ufinyu wa Bajeti unaopelekea kutotekeleza baadhi ya shuguli muhimu na kutowafikia walengwa wote.
Mwamko mdogo wa Vijana na Wanawake kuanzisha shughuli za uchumi na kujiwekea akiba.
Imani za kishirikina zinazozuia watu kujenga Nyumba bora.
Watu kutopenda kazi za kujitolea.
Mila na desturi zenye madhara katika jamii zinazopelekea maambukizi ya VVU.
Unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU ambao unakwamisha watu kutokujitokeza kupima afya na hivyo kukwamisha juhudi za mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI
Baadhi ya Vikundi kutokurejesha mkopo kwa wakati kulingana na muda wa mkataba.
Baadhi ya wanajamii kuwaficha majumbani watu wenye ulemavu
Ufumbuzi
Matarajiio
Kuhamasisha kuanzisha vikundi vya Vikoba katika vijiji, kaya na watumishi kutoka 90 hadi kufikia vikundi 100 Mwaka 2017.
Halmashauri kuendelea kutoa asilimia 10 za kusaidia mifuko ya Wanawake na Vijana.
Kutoa Elimu kwa wakopaji juu ya urejeshaji wa Mikopo na Elimu juu ya faida zitokanazo na Mikopo.
Halmashauri kuajili Maafisa Maendeleo ya Jamii wakutosha katika Kata na Vijiji.
Halmashauri kununua Vitendea kazi vya kutosha na kujenga ofisi.
Halmashauri na Serikali kuu kutenga Fedha za kutosha kwa Watumishi wa Maendeleo ya Jamii.
Kutoa Elimu kwa wakopaji juu ya urejeshaji wa Mikopo na Elimu juu ya faida zitokanazo na Mikopo.
Kusimamia sheria zinazowabana waliokopa kurejesha kwa wakati.
Kuongeza uhamasishaji jamii kutumia vipato vyao kujijengea nyumba bora.
Halmashauri kuendelea kutenga fedha za mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa