PICHA |
JINA KAMILI |
CHEO |
NAMBA YA SIMU |
BARUA PEPE |
|
Dr. Rainer Kapinga | Mku wa idara ya afya na ustawi wa jamii
|
0782272190 | kapingar@gmail.com
|
UTANGULIZI
Idara ya Afya ni miongoni mwa idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge. Idara ya Afya inatekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Huduma hizi zimekuwa zikitolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya na kwa njia ya mkoba katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri. Katika Halmashauri kuna jumla ya vituo 34 vya kutolea huduma za afya. Vituo hivi vinamilikiwa na serikali na mashirika ya dini. Vituo vya kutolea huduma za Afya vinavyomilikiwa na serikali ni 27, 7 vinamilikiwa na mashirika ya dini. Kati ya vituo hivyo 45, kuna hospitali 1, vituo vya Afya 3 na zahanati 30. Idara hii ina jumla ya watumishi 324.
Idara ya Afya inatekeleza majukumu makuu mawili abayo ni Afya kinga na Afya tiba. Kupitia Afya tiba idara imelenga kutoa matibabu sahihi kwa gharama nafuu kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge. Afya kinga imelenga kuwakinga wananchi wasipate magonjwa yale ya kuambukiza, yasiyoyakuambukiza pamoja na kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Idara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa afya wa V wa mwaka 2015 -2020. Katika kuhakikisha wananchi wanapata tiba sahihi, idara imekuwa ikitekeleza majukumu yafuatayo:
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa