Na.Anna Kapama_Sikonge
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imevuka lengo katika Zoezi la Sensa ya watu na Makazi kwa kuhesabu zaidi ya Idadi iliyokadiriwa na kufikia zaidi ya asilimia miamoja.
Mhe.Palingo ametoa kauli hiyo katika Mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri na kuwapongeza waliohusika kufanikisha zoezi hilo.
"Katika Zoezi la Sensa linaloendelea niwapongeze Kamati zote Kuanzia Kamati ya Wilaya, Kata, Vijiji na Vitongoji kwa kuandaa vizuri zoezi la Sensa, tulikuwa na Makisio ya kaya 41,105, mpaka Jana tumefikia Kaya 53,874 sawa na 131.1% na bado tunaendelea kuhesabu" alifafanua zaidi
Aidha, DC Palingo ameongeza kuwa Serikali imeongeza Siku Saba ili kutoa nafasi kwa ambao hawakuheaabiwa wahesabiwe.
"Tuendelee kutoa Ushirikiano ili tumalizie zoezi hili Vizuri,kila mtu apate nafasi ya kuhesabiwa, zoezi la kudodosa Majengo lilianza Jana na linaendelea pia kwa siku tatu"DC Palingo akifafanua.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa