Na Edigar Nkilabo – Sikonge DC
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Seif Salum amesema watumiaji wote wa mazao ya misitu hasa kuni wanapaswa kulipa tozo za kuni kwa mujibu wa sheria ya msitu na kanuni zake ambapo ujazo wa mita cubic 1tozo ni shilingi elfu sita mia tano (6500/=).
Akizungumza katika kikao cha kujadili ulipaji tozo za kuni kwa wadau wa mazao ya misitu Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amesema kikoa cha leo kimetoa suluhu ya mkwamo wa ulipaji wa tozo za kuni.
“Serikali imetoa mwongozo na utaratibu wa kutumia mazao ya misitu, mfano nyie wakulima wa tumbaku mnatumia kuni nyingi ni muhimu kulipa hizo tozo za kuni kulingana na kiwango ulichotumia”
“Fedha hizi mnapolipa baadae zinarudi kwenu tena katika shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo unapolipa hizi tozo ni uzalendo na unapaswa kujivunia maendeleo yanayopatikana”aliongeza.
Aidha Ndugu Seif amesisitiza kuwa Halmashauri kwa kushirikiana na taasisi zingne wataendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa kuni wakiwemo wakulima wa tumbaku,wanaochoma tofali na kutumia kuni kwa wingi ili kuepuka mkwamo wa ulipaji wa tozo za kuni.
Kwa upande wake Mhifadhi kutoka Wakala wa Misitu Tanzania(TFS), Eleuter Kibiki amewataka wananchi wote kufuata sheria na utaratibu wakati wa kuvuna misitu hata kama misitu hiyo ni mali yao wanapaswa kuzingatia utaratibu wa kupata kibali cha kutumia.
“Watu wengi wanakata miti kiholela hawafuati taratibu na bado mlio wengi mnakwepa kulipa tozo za mazao ya misitu jambo ambalo ni kinume na sheria”alisema Bw.Kibiki.
Aidha Mhifadhi wa TFS amewataka wakulima wa tumbaku kuipanda miche yote wanayopewa na kuitunza ili ikue na kuwa na nishati endelevu ya kuni badala ya kutegemea miti ya asili pekee kwa ajili ya kupata kuni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ushirika – Jukwwaa Sikonge, Shaban Gambo amesema wamepokea maelekezo yote ya serikali watakaporudi katika maeneo yao watatoa elimu kwa wakulima wenzao na kusisitiza ulipaji wa tozo za kuni ili wananchi na serikali kwa pamoja waweze kunufaika.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa