Na Edigar Nkilabo - Sikonge DC.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.Thomas Myinga ametoa wito kwa wananchi wa Sikonge kujitokeza kwa wingi na kwenda kushiriki zoezi la upigaji kura kwa kuwachagua viongozi wanaowataka pasipo wasiwasi kwakuwa serikali imeimarisha usalama wa raia na itaendelea kuimarisha usalama hata baada ya uchaguzi mkuu kama siku zote.
Mhe.Myinga ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya Habari katika Ofisi za Wilaya ambapo amewahakikishia usalama wananchi wote watakaoenda vituoni kupiga kura Oktoba 29, mwaka huu.
“Kwenye Wilaya yetu tunavituo vya kupigia kura 451 na vyote vitatumika niwatoe wasiwasi serikali imeimarisha usalama kama siku zote hivyo nendeni mkashiriki katika zoezi la kupiga kura mchague viongozi mnao wataka kulingana na sera zao walizotoa wakati wa kampeni”
“Pia ukishamaliza kupiga kura wewe rudi nyumbani kapumzike usubiri matokeo suala la ulinzi wa kura tuwaachie waliopewa jukumu hilo ambao ni mawakala wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu”aliongeza Mhe.Myinga.
Kwaupande wake Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Sikonge Mwl. Benjamin Mshandete amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100 kwakuwa tayari wameshapokea vifaa vyote na kuvisambaza kwenye maeneo ya kata.
“Wale wote ewaliojiandikisha kupiga kura na wanavitambulisho wajitokeze wakatimize haki yao ya kikatiba kwakuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeandaa mazingira bora kwa wananchi kupiga kura”alisema.
Aidha Mshandete amesema tayari wamekamilisha mafunzo kwa Makarani waongozaji wapiga kura pamoja na Wasimamizi wa vituo na Wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura ambao watapelekwa kwenye vituo vyote 451.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa