Na. Robert Magaka – Ipembampazi,Sikonge – Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ameongoza kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya kukagua ukarabati wa miundombinu ya Barabara ya Rungwa Ipole kilomita 172.
Katika ziara hiyo Mhe. Chacha amekagua ujenzi wa Daraja mita 10 na ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami mita 600 katika kitongoji cha Mkola Kata ya Ngoywa.” Fanyeni Haraka Daraja hili likamilike kwa wakati ili lihudumie wananchi wanaotumia njia hii” amesema DC. Chacha.
Kwa upande wake Bw. Amos Tano Mhandisi wa Ujenzi toka Tanroads Tabora amemuhakikishia Mhe. Chacha kuwa Mkadarasi yupo eneo la kazi na kazi inaendelea hivyo kufikia mwishoni kwa mwezi Machi ujenzi huo utakuwa umekamilika ingawa tayari Mkandarasi kashatengeneza pitio la pembeni kurahisisha mawasiliano ya Barabara hiyo ya Rungwa – Ipole.
Aidha Mhe. Chacha amezuru eneo ambalo abiria wa Basi la Kingalu Express linalofanya safari zake toka Tabora kwenda Mbeya lenye namba T 267 AWG waliokwama leo na kuwapa pole lakini ameagiza Uongozi wa Tanroads kutuma Gari haraka ili kuwaondoa abiria hao katika eneo hilo la hifadhi ya Ipembampazi kilomita 54 toka Ipole.
Vilevile Mhe. Chacha amefika katika eneo lingine la Barabara hiyo ya Rungwa – Ipole katika mbuga ya Ipembampazi ambalo pia limeathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha lililopo kilomita 64 toka Ipole.
Mhe. Chacha amehitimisha ziara hiyo kwa kutoa maelezo ya kuharakisha ukarabati wa Barabara hiyo muhimu kwa mawasiliano ya watu ili shughuli za kijamii na kiuchumi zisikwame.
Sikonge Hakuna kilichosimama! Uongozi wa Vitendo,Kazi Iendelee.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa