Na Anastazia Maguha – SikongeDC,
Shule ya Sekondari Sikonge imepokea kompyuta 17 na Kompyuta mpakato 1 ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza somo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),kwa vitendo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa vifaa hivyo,Mwalimu wa TEHAMA Bi.Cecilia John,amesema wamepokea vifaa hivyo siku ya Ijumaa na jana wametembelewa na jopo la Wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Sikonge kwaajili ya kukagua vifaa hivyo.Jopo hilo lilijumuisha Afisa Elimu Sekondari, Wahasibu, Afisa TEHAMA na Mafundi.
Alisema anaishukuru Halmashauri kwa kupewa vifaa hivyo ambavo vitawezesha ufundishaji.
"Nashukuru sana Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa sababu mara ya kwanza nilikua nafundisha kwa nadharia ila sasa vifaa hivi vitaniwezesha kuwafundisha Wanafunzi kwa vitendo"
Aliongeza ; Kompyuta hizi hazitakuwa msaada kwa Wanafunzi wanaojifunza TEHAMA pekee bali kwa Wanafunzi wote kwa sababu tupo dunia ya Sayansi na Teknolojia ambapo taarifa zote zinapatikana mtandaoni.
Nao Wanafunzi wa Kidato cha tano Moses Pawa na Aisha Mohammed wa Sikonge Sekondari wamesema Kompyuta hizo zitawawezesha kupakua mada mbalimbali wakati wa vipindi na wakati wa kujisomea.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa