Na Edigar Nkilabo – Sikonge DC
Kamati ya Usalama ya wilaya ya Sikonge leo tarehe 17 Novemba,2025 imefanya ziara ya kukagua miradi ya elimu na afya inayotekelezwa katika kata za Kitunda na Kiloli zilizopo tarafa ya Kiwere wilayani Sikonge.
Ziara hiyo ikiongozwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bi.Rozina Swai ambapo ameeleza kuwa kamati ya usalama imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi iliyotembelewa ikiwemo mradi wa ujenzi wa shule shikizi Kona Nne (04) iliyopo kijiji cha Kapumpa kata ya Kitunda mradi ambao unaojumuisha Madarsa manne,Ofisi mbili na matundu manne ya vyoo ambapo imegharimu shilingi milioni 75.
“Niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa mradi huu kwa kuwa tayari umekamilika watoto wetu wataanza kutumia madarasa haya na kuepuka kutembea umbali mrefu kwenda shule mama ya Kapumpa lakini pia naamini hata idadi ya wanafunzi itaongezeka na utoro ndiyo basi tena”alisema Bi.Rozina Swai.
Aidha Bi.Swai amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Selemani Pandawe na Menejimenti ya Halmashauri kwa ubunifu na mawazo ya kubadili mradi wa ujenzi wa Zahanati na kuamua mradi huo uwe wa wodi ya wanaume na wanawake kufuatia ufadhili wa Wadau wa maendeleo kutoka Jakaya Mrisho Kikwete Foundation ambao wameamua kujenga Zahanati na Nyumba za Watumishi.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Selemani Pandawe amesema lengo la kubadili mradi huo na kujenga wodi ni kuepuka uwepo wa miradi miwili inayofanana na badala yake Halmashauri imeamua kuweka wodi ikiwa ni maandalizi ya kuweka Kituo cha Afya cha Kata ya Kiloli kwa kuwa kata hiyo haina kituo cha afya.
“Ni sera ya serikali kila kijiji kuwa na Zahanati na kila kata kuwa na Kituo cha AFya hivyo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa wodi, nyumba ya watumishi na jengo la Zahanati itakuwa rahisi kuifanya kituo cha afya na kuongeza wigo wa utoaji huduma kwa wananchi”alisema.
Kamati ya Usalama imekagua Jumla ya miradi mitatu ikiwemo miwili ya elimu ya ujenzi wa shule shikizi Kona Nne iliyopo kata ya kitunda, Shule shikizi kona Moja iliyopo kata ya Kiloli na Zahanati ya Ipembe iliyopo Kiloli.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa