Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Mhe. Cornel Lucas Magembe, ameongoza kikao cha afya ya msingi kilicholenga kuweka mikakati ya uwagawaji wa dawa za kingatiba kwa mwaka 2024. Kikao hicho kimejadili hatua muhimu za kuhakikisha watoto wanapata matibabu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Bi. Grace Mollel, akimwakilisha Mganga Mkuu wa Wilaya, amesema kuwa wilaya ya Sikonge inatarajia kuwafikia watoto 48,698 wenye umri wa miaka 5 hadi 14. Hii ni hatua muhimu katika kudhibiti magonjwa ambayo yanawaathiri watoto, na hivyo kuimarisha afya ya jamii nzima.
Katika hotuba yake, Mhe. Magembe ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo, akisisitiza umuhimu wa afya kwa maendeleo ya nchi. Amesema kuwa, "Hakikisheni watoto wanapata chakula kabla ya kuwapatia kingatiba hizo muhimu, tushikamane wote ili tufikie malengo ya kulinda watoto wetu na jamii nzima na kadhia ya maradhi haya ya minyoo ya tumbo na kichocho.”
Zoezi la utoaji kingatiba linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia Septemba 23 hadi 24 mwaka 2024. Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni miongoni mwa magonjwa 21 yanayoathiri mamilioni ya watu duniani, na husababisha madhara makubwa, ikiwemo utapiamlo na kushindwa kuhudhuria masomo kwa watoto.
Bottom of Form
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa