WASITISHIWA MKATABA UJENZI HOSPITAL YA WILAYA SIKONGE
Kuu ya Wilaya ya Sikonge yafanya maamuzi ya kuondoa mkataba kwa mafundi waliokabidhiwa jengo la Utawala na jengo la wagonjwa wa nje (OPD).
Maamuzi hayo yalitolewa baada ya Mafundi hao kufanya kazi kwa kusuasua huku sababu moja wapo ikiwa ni ucheleweshwaji wa kukabidhi kazi kwa wakati huku kukiwa na tuhuma mbalimbali za uharibifu wa vifaa vya ujenzi huku kukiwa na kutoelewana kati ya mafundi hao jambo lililopelekea migomo ya hapa na pale na kuchangia kazi kutoenda kwa wakati.
Akitoa maamuzi hayo Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alisema kuwa Jofrey Msemwa wa jengo la wagonjwa wa nje na Ally Ajji wa jengo Utawala hawataongezwa mkataba mwingine kwani wameshindwa kufanya kazi ilivyotakiwa, 5 hivyo basi nafasi hizo zipo wazi na mafundi wenye uwezo wanashauriwa kuomba kujaza nafasi hizo mara utaratibu utakapotangazwa.
Pamoja na maamuzi hayo mafundi waliositishiwa mkataba watalipwa stahiki zao kulingana na kazi waliyoifanya. Na endapo kuna uharibifu wowote uliofanya pesa zitakatwa ili kufidia mapungufu hayo.
“hatutokubali fundi unapewa kazi tena ya serikali alafu unafanya kazi kwa kiwango cha chini, ni kwanini msiwe na huruma kwa watanzania tunaotegemea kuyatumia majengo haya” alisema Mkuu wa Wilaya.
Sanjari na hayo pia walitoa onyo kwa Fundi wa jengo la mama na mtoto kujitahidi kuendana na muda na kuhakikisha kuwa wanakabidhi majengo hayo mwisho wa mwezi wa sita ama sivyo hatua zitaendelewa kuchukuliwa ikiwemo kupatiwa fundi ne wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo.
Jengo la wagonjwa wa nje OPD likiwa katika hatua ya upauaji.
Akitoa ufafanuzi wa kisheria bwana Pascal Kapinga ambaye ni Mwanasheria wa Halmashauri alisema kuwa Wilaya haijasitisha mikataba kwa mafundi hao isipokuwa kilichofanyika ni kutowaongeza muda wa mkataba mwingine kwani mkataba wao wa mwanzo ulikuwa umeisha tokea mwezi wa tano 5.
Naye Mkurugenzi Mtendaji (W) Martha Luleka aliongezea kuwa mafundi hao wasichukulie jambo hilo kwa mawazo hasi kwani Wilaya imejaribu kuwavumilia kwa muda mrefu ikiwemo kukaa pamoja na kuwashauri kuandaa mpango kazi lakini mara zote hawakufata ushauri uliotolewa . Hivyo alishauri wakati mwingine watakapopewa kazi wafanye vizuri.
Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Sikonge ilipokea kiasi cha Tsh. Bilioni moja na moilioni mia tano kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ambapo kwa hatua za awali kuwejengwa majengo saba na hatua ya ujenzi imefikia kwenye upigwaji lipu kwa baadhi ya majengo na majengo mengine yanaendelea na hatua za upauaji huku ikitegemewa kukabidhiwa mwishoni mwa mwezi wa Sita.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa