WANASIKONGE WANUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI.
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge yatoa mkopo wa Tsh. Mil 88 kwa vikundi vya Wakinamama, vijana na Walemavu.
Mikopo hiyo isiyo na riba ilitolewa na Mkurugenzi Mtendji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Martha Luleka ambapo mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh. Mil 88 ilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Peter Nzalalila kwa ajili ya kuwakabidhi wanavikundi hao waliokusanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Ufundi FDC na tayari mikopo ilishaingizwa kwenye akaunti za kila kikundi.
Akitoa elimu ya ujasiliamali kwa wanavikundi wanufaika wa mikopo hiyo, Bi. Martha alisema ni vyema vikundi vikafanya bishara ya pamoja ambayo itakuwa rahisi kuiendesha. Aliongeza kuwa kufanya biashara moja kama kikundi itasaidia kuwepo kwa nidhamu ya matumizi ya fedha kuliko kila mtu atakapofanya biashara ya peke yake.
Aliyasema alipokuwa akitoa elimu ya ujasiliamali kwa wanufaika wa mkopo huo na kuongeza kuwa endapo fulsa zilizopo zitatumiwa vizuri na wanavikundi hao zitawasaidia kuwanyanyua kiuchumi, kwani Halmashauri inategemea kuona mabadiliko kwa wanufaika hao ya kiuchumi na kifikra.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sikonge Martha Luleka aliyesimama katikati akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Peter Nzalalila mfano wa Hundi ya mkopo kwa ajili ya kuwakabidhi vikundi vya wajasiliamali.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila alipokuwa akikabidhi mfano wa hundi ya mkopo kwa makundi hayo, alitoa nasaha zake kwa vijana kuanzisha biashara eneo linalofahamika na lenye fulsa mbalimbali ili kuwakwamua kiuchumi vile vile aliwataka kutumia wataalamu wa maendeleo ya jamii ambao wanapatikana katika Halmashauri ili kupata ushauri wa namna ya kuanzisha miradi mbalimbali, huku akitoa wito kwa makundi yote kurudisha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze kutumika kukopesha vikundi vingine.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Sikonge imekuwa ikitoa mikopo isiyokuwa na riba kwa makundi ya vijana, wanawake na walemavu ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa