WALIMU WILAYANI SIKONGE WAPEWA MAFUNZO.
Walimu wa shule za msingi wilayani Sikonge wamepewa mafunzo mahalumu ya usajili wa wanafunzi kupitia mfumo wa( EQUIP) iliyoboreshwa.
Mafunzo hayo haayo yalitolewa na wawezeshaji kutoka OR TAMISEMI yalifanyika katika shule ya msingi Sikonge. Lengo likiwa ni kuisaidia serikali kupitia wizara ya elimu kupata raarifa sahii juu ya maendeleo ya wanafunzi na walimu husika katika kila shule.
Mafunzo hayo yatawawezesha walimu wakuu kupata weredi namna ya kujaza taarifa za mwanafunzi na mwalimu wake katika kila somo husika. Pia kupata maendeleo ya shule zote zilizounganishwa katika mpango maalumu. Hivyo kutoa takwimu sahihi kwa TAMISEMI.
HABARI PICHA
Wajumbe wakisikiliza kwa makini maelekezo.
Akitolea ufafanuzi kiongozi wa wawezeshaji kutoka TAMISEMI Bwana Sweetbeth Kashaija alisema kuwa ‘ hatua hii ni namna ambayo mwalimu mkuu atakavyotumia hizi takwimu katika kusimamia na kuendesha shule yake’’ pia aliongeza ‘’ mafunzo yamekuwa ya ufanisi mkubwa ukitegemea na awali ambapo kwa sasa walimu wakuu wote wameweza kuingiza taarifa na shule zote 95 zilizopo katika halimashauri ya wilaya ya sikonge zimeweza kutuma taarifa kwenye seva ya TAMISEMI na tunaimani namna walivyoshiriki na changamoto zote tumezitatua’’.
Akielezea miongoni mwa changamoto zilizokuwa zikiwakabili walimu wakuu wa shule ni pamoja na maharifa haba wa namna ya kutumia mfumo huo swala ambalo limetatuliwa na walimu wamepewa nyenzo zitakazowasaidia hata kama itatokea mwalimu mgeni akaletwa katika shule, mwongozo ule utawasaidia.
Vilevile mwalimu mkuu wa shule ya msingi ndugu Dickison Alfredy alisema kuwa ‘’ sisi kama wakuu wa shule mfumo huu utatusaidia kutuma taharifa zetu kwa usahihi na kuzifikisha taarifa mahali husika.’’ Kauli hii iliungwa mkono na wajumbe wa mafunzo hayo na kuahidi kuutumia ujuzi waliopewa kufanikisha zoezi hili.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa