Na Linah Rwambali
Bodi ya maji ya bonde la Ziwa Tanganyika imefanya mkutano na wadau wa maji katika Wilaya ya Sikonge ili kujadili na kuweka mipango ya pamoja ya kuhifadhi vyanzo vya maji.
Katika mkutano huo, vyanzo vya maji ambavyo vilijadiliwa vilikua ni bwawa la Igumila na bwawa la Urua yaliyopo katika Wilaya hiyo.
Aidha, katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Cornel Magembe ambaye alikua mgeni rasmi aliipongeza bodi kwa kuandaa mkutano huo na aliwaelekeza wadau wote waliohudhuria kufuatilia kwa makini yote watakayojadili.
“Niwapongeze bodi ya maji ya bonde la Ziwa Tanganyika kwa kuandaa jukwaa la wadau wa maji kwani utunzaji wa maji utatuhakikishia upatikanaji endelevu wa maji” alisema.
“Nawaelekeza viongozi wote wa vijiji na Kata pamoja na washiriki wote kutoa ushirikiano wa kutosha ili zoezi lifanyike kikamilifu na hatimaye mkatoe elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji katika maeneo yenu” alisema Magembe.
Naye Mwenyekiti wa jukwaa la wadau wa bodi ya maji ya bonde la Ziwa Tanganyika Paschal Ngunda alisema vyanzo vyote vya maji huwa safi baada ya kutengenezwa na wataalamu ila kwa kadri muda unavyozidi kwenda maji huchafuka siku hadi siku. Kila mdau ashiriki vyema katika utunzaji wa maji kwani mustakabali wa maji ni sisi wadau” alisema.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe.Gasto Lwambano alisema bwawa la Igumila lipo katika Kata ya Kiloleli na kuna changamoto katika utunzaji wa bwawa la Igumila. Hivyo anashukuru kwa elimu na majadiliano yaliyofanyika kwani yatawawezesha wananchi kutunza maji ipasavyo na hatimaye kusaidia upatikanaji wa maji ambao ni endelevu.
Mkutano huo umejumuisha Madiwani, Watendaji wa kata na vijiji pamoja na wataalamu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa