SIKONGE - UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA KUKAMILIKA NDANI YA MWEZI MMOJA.
NA EVELINA ODEMBA
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge yaagizwa kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ndani ya mwezi mmoja .
Agizo ilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Agrey Mwanri alipotembelea ujenzi wa mradi huo na kukuta ukiwa katika hatua mbalimbali ikiwemo hatua ya uezekaji paa kwa baadhi ya majengo wakati majengo mengine yakiwa katikaa hatua ya upigwaji lipu.
Akiwa wilayani hapo Mhe. Mwanri alisema jitihada za dhati zitumike kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya siku alizoagiza ambapo alitembelea mradi huo tarehe 26 mwezi wa 6 mwaka 2019 kusema kuwa hadi kufikia ataehe 26 mwezi wa 7 mwaka 2019 majengo hayo yawe yamekamilika na kukabidhiwa hivyo alitaka kufungwa kwa umeme wa jenereta ili kuruhusu mafundi kufanya kazi usiku na mchana ili kukimbizana na muda.
Ujenzi huo unategemea kutumia bilioni 1.5 hadi kukamilika kwake, pesa ambazo zimetolewa na Serikali ya awamu ya tano chini ya raisi Joseph Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo saba ya awali ambapo ndani ya majengo hayo ni Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la kufulia, jengo la mionzi, jengo na mama na mtoto, jengo la maabala, jengo la dawa pamoja na jengo la utawala.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Agrey Mwanri aliyevaa shati jeupe, Mkuu wa Wilaya Mhe. Peres Magiri mwenye suti nyeusi na Mkurugenzi Mtendaji Martha Luleka pamoja na wataalamu wakitoka kukagua jengo la mama na mtoto katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya Sikonge.
Aidha aliagiza kukatwa kwa mishahara ya wajumbe kamati ya mapokezi ya vifaa vya ujenzi wa hospitali hiyo ambao pia ni watumishi wa Halmashauri kutokana na kuwepo kwa madai ya baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kutotosheleza mahitaji. Hivyo alitaka kuundwe tume ya kuchunguzwa madai hayo na ikionekana kuna tatizo watumishi hao wakatwe mishahara yao ili kufidishia mapungufu hayo
Sanjari na hayo pia aliitaka kampuni iliyopewa jukumu la kulinda vifaa vya ujenzi wa hospitali hiyo kuchukuliwa hatua mara moja kutokana na kuwepo kwa wizi wa baadhi ya vifaa ikiwemo nondo 90.
“kampuni hiyo ilipe fidia ya upotevu wa mali hizo na ichukuliwe hatua mara moja, hii haiwezi kuwa hasara ya Halmashauri ni lazima sheria zifuatwe” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Marha Luleka alipokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kama ilivyoagizwa huku akishukuru kuongezewa kwa muda huo kuwa kutawezesha kazi kukamilika kwa vizuri. Sanjari na hayo pia aliwashukuru wadau mbalimbali wa maendeleo Sikonge ambao wameweza kujitolea kufanikisha ujenzi wa Hospitali hiyo ikiwa ni njia ya kuunga mkono serikali ya Awamu ya Tano.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa