Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Selemani Pandawe ameongoza timu ya menejimenti ya Halmashauri kukagua mradi wa kituo cha Afya Igigwa ambacho ujenzi upo hatua za mwisho za umaliziaji,Wataalam walioambatana na Mkurugenzi wameshauri umaliziaji uharakishwe ili wananchi waanze kupata huduma za afya katika kituo hicho.
Kwa upande wa ujenzi wa stendi ya mabasi unaohusisha ujenzi wa matundu ya sita ya vyoo pamoja na banda la kupumzikia abiria umefika asilimia 98%, Pandawe ameagiza marekebisho yote waliyopendekezwa na watalaam toka divisheni na vitengo mbalimbali yafanyiwe kazi haraka ili stendi hiyo ianze kufanya kazi.
Vilevile Mkurugenzi amefika katika shule ya Sekondari Chabutwa kuona utekelezaji wa agizo lake la kufanya marekebisho ya mashimo ya maji taka ya vyoo vya Walimu na wanafunzi iwapo limetekelezwa.Hali ni nzuri vyoo vipo safi hivyo imeondoa shaka ya shule kufungwa kutokana na ukosefu wa huduma ya choo shuleni hapo.
JENGO LA MAMA NA MTOTO KITUO CHA AFYA IGIGWA.
JENGO LA OPD.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa