SIKONGE YATOA TUZO KWA KATA KINARA WA MAPATO 2018/2019
Na EVELINA ODEMBA
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge yatoa Tuzo kwa Watendaji wa Kata zilizofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bi. Martha Luleka, ikiwa ni mara ya kwanza kwa jambo hili kufanyika Wilayani hapa zilikabidhiwa kwa vinara wa Kata hizo na mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Mhe. Musalika Robert Makungu.
Muandaaji wa Tuzo hizo Bi. Martha alieleza kuwa licha ya jambo hilo kuwa pongezi kwa Kata zilizofanya vizuri vilevile limelenga kuwa motisha kwa Kata zingine kujitahidi kufikia makisio waliyopatiwa na hata kuvuka lengo kwani mkakati wa Halmashauri yake ni kukusanya mapato kutoka 87% zilizokusanywa mwaka wa fedha 2018/2018 na kufikia 100% kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na jambo hilo linawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza majukumu kwa weredi.
Naye mgeni rasmi Mhe. Makungu aliongeza kuwa jambo hilo linawezekana ikiwa tu viongozi na watu wanaowaongoza watazungumza lugha moja. Hii ikiwa na maana kuwa mikakati yote waliyoiweka ikizingatiwa Sikonge itavuka lengo la 100% kutokana na kuwa Wilaya hii ina vyanzo vingi vya mapato pamoja na watu wachapakazi hivyo aliendelea kusisitiza kuwa nyenzo hizi zikitumiwa vizuri zitatoa matokeo bora.
Tuzo hizi ziligawanyika katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza lilikuwa ni Tuzo kwa Kata zilizokusanya mapato mengi zaidi. Katika kundi hili zawadi zilitolewa kwa washindi watatu na mshindi wa kwanza alikuwa kata ya Kipili iliyokusanya Ml. 76 sawa na 107%, kata ya pili ilikuwa Kiloli iliyokusanya Ml. 70 sawa na 121.9% wakati kata ya Nyahua ikiwa mshindi wa tatu kwa kukusanya Ml. 66 sawaa na 172.8%. Asilimia hizi zilikokotolewa kulingana na makisio yaliyowekwa kwa kata hizo.
Vilevile kundi la pili ilikuwa ni tuzo kwa kata zilizovuka malengo na kukusanya kiasi kikubwa zaidi ya makisio waliyowekewa. Ambapo katika Tuzo hizi kata ya Sikonge iliibuka mshindi wa kwanza ikiwa imekusanya 279.4%, ikifuatiwa na Kata ya Kiloleli 273.1% wakati kataa ya tatu ikiwa Mkolye 215.9%.
Sanjari na ugawaji wa Tuzo hizo ambazo ziliuzuliwa na Viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya, pia watendaji wa kata na vijiji walipatiwa semina ya kiutendaji ili kuwaongezea ufanisi kazini. Semina hiyo ilikuwa shirikishi ambapo majadiriano mbalimbali yalifanyika.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa