Na Edigar Nkilabo, Sikonge
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imepata Hati inayoridhisha baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali CAG kukagua na kuridhishwa na taarifa za fedha ambazo zimeandaliwa kwa usahihi na kwa kuzingatia viwango vya uhasibu vya kimataifa vya uandaaji wa taarifa za fedha (IPSAS)
Akizungumza Wilayani Sikonge katika kikao maalum cha Kamati ya fedha,uongozi na mipango kupitia utekelezaji wa hoja za ukaguzi wa hesabu za mwaka 2023/2024 Mkaguzi Mkuu wa Nje mkoa wa Tabora Hamza Zonga amesema hati hiyo imetolewa na CAG kwa kuwa hakuna jambo lolote kubwa lililobainika na mkaguzi kumfanya atoe hati yenye shaka.
“Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ilifanyiwa ukaguzi wa Hesabu na CAG kwa mwaka ulioishia tarehe 30Juni, 2024 na kupata hati inayoridhisha hata hivyo haimaanishi kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ina mfumo wa udhibiti wa ndani wenye ufanisi wa asilimia mia moja”amesema.
Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Tabora Dkt.John Mboya amewataka wakuu wa Idara na vitengo kutoa ushirikiano kwa mtunza hazina DT na mkaguzi wa ndani DIA
“Nimeona taarifa ya ukaguzi wa mwaka 2023/2024 ilikuwa na jumla ya mapendekezo 46 yaliyokuwa yakihitaji ufuatiliaji.Mapendekezo haya yanajumuisha mapendekezo ya hoja 29 zilizoibuliwa katika ukaguzi wa hesabu wa mwaka 2023/2024 na hoja 17 za mwaka wa nyuma katika utekelezaji naona mapendekezo 11 sawa na asilimia 24 yametekelezwa, mapendekezo 35 sawa na asilimia 76 yapo katika utekelezaji hivyo niaagize wataalamu kushirikiana na DT kikamilifu kujibu hoja sio mnaachia wasaidizi wenu”alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe.Rashid Magope amesema hati inayoridhisha imetokana na utendaji mzuri wa wataalamu katika kusimamia matumizi sahihi ya fedha..
“Nawapongeza wataalamu wetu wamekusanya mapato kwa asilimia 98 hadi mwezi Mei, vivyo hivyo kwenye matumizi wamekuwa wakisimamia matumizi sahihi na kuwezesha hati inayoridhisha licha wa uwepo wa changamoto ndogo ndogo”alisema.
Naye mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe.Paul Chacha amesema watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa nidhamu na ushirikiano ili kumaliza hoja zilizosalia, si jambo jema kubaki na hoja ambazo zinaweza kufungwa kama zitajibiwa kwa usahihi.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa