Na Linah Rwambali
Vifo vya mama na mtoto vimepungua Wilayani Sikonge kutokana na juhudi za serikali katika kuboresha huduma za Afya.
Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Cornel Magembe wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa kipindi cha kuanzia Julai 2024 hadi Juni 2025.
“Serikali imeendelea kupambana na vifo vya mama na watoto ambapo hadi sasa, vifo vimepungua toka 74% hadi 43% ” amesema.
“Hii ni kutokana na juhudi za Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan za kuleta vituo vya Afya kwenye maeneo mengi na kuhakikisha anaajiri watumishi katika vituo hivyo” amesema Magembe.
Kwa niaba ya madiwani wote, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao.
“Tunakushukuru Mhe Mkuu wa Wilaya kwa jinsi tulivyofanya kazi kwa upendo,changamoto ilipotokea tuliitana ofisini na kujadili. Kwa niaba ya Baraza la madiwani, nikushukuru kwa hilo” amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sikonge Bi Anna Chambala amewapongeza watumishi kwa kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wao na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa