Wataalam wa afya ngazi ya wilaya wametembelea zahanati ya kijiji cha Igalula,kata ya Sikonge kufuatilia utekelezaji wa kampeni ya utoaji wa matone ya vitamin A pamoja na upimaji wa hali ya lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Mratibu wa afya ya mama na mtoto wilaya ya Sikonge Bi. Lenatha Mondo amesema wilaya ya Sikonge inakusudia kutoa matone ya vitamin A kwa watoto 60,677 ifikapo Juni 30 mwaka huu.
Mpaka sasa Wilaya ya Sikonge imekwisha toa matone ya vitamin A kwa watoto 55,434 katika vituo arobaini vya kutolea huduma za afya pamoja na huduma mkoba ikiwa ni asilimia 90 ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Kampeni hii ya utoaji wa matone ya vitamin A pamoja na kupima hali ya lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ilianza Juni 1, 2024 na itarajiwa kufikia kikomo ifikapo Juni 30, 2024.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa