Sikonge_Tabora
12.10.2022
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Seleman Pandawe ameitisha kikao na Viongozi na wasimamizi wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 29 katika shule za Sekondari 9 za Wilaya ya Sikonge wakiwemo Watendaji wa Kata, na Walimu Wakuu kwa ajili ya kuwapa maelekezo ya namna Bora ya utekelezaji wa Miradi hiyo ikiwa ni maandalizi ya Mapokezi ya Wanafunzi wa kidato Cha kwanza Mwaka wa Masomo 2023.
Awali akifungua kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji Seleman Pandawe amewataka walimu Wakuu kuwashirikisha wananchi ambao ni wadau wa Maendeleo kwa kutoa taarifa ya Miradi na thamani ya fedha za miradi inayotekelezwa katika maeneo husika ili wafahamu Serikali inachokifanya kwa wananchi wake.
Aidha,DED Pandawe amewasisitiza kujiepusha na matumizi mabaya ya fedha na badala yake wawe waaminifu ili miradi iweze kukamilika kwa Ubora na Kwa wakati.
"Kila mtu anahitaji fedha,lakini siyo kila fedha utahitaji kutumia, zingine ziache zifanye shughuli zilizopangiwa" DED Pandawe
Kwa Upande wake Afisa wa TAKUKURU Wilaya ya sikonge Magore Msena amewasisitiza kuwa wazalendo wakizingatia Sheria na taratibu zilizowekwa katika utekelezaji wa Miradi hiyo.
"Tusihamasishane kukwamisha hii miradi, maelekezo yanapotolewa wakati wa Ujenzi yafanyiwe kazi kabla ya kuendelea na kazi nyingine, tuwe wazalendo kukamilisha miradi" Magore Msena
Katika hatua nyingine , Afisa Manunuzi Wilaya ya Sikonge Shadrack Baruti amesisitiza taratibu za Manunuzi kuzingatiwa kwa uwazi.
"Kuna baadhi ya walimu wanaenda kufanya kotesheni bila kushirikisha Kamati zote za Ujenzi , siyo utaratibu , Vifaa vikija vikaguliwe na Kamati msifanye kimyakimya, fanyeni kazi kwa uwazi" Baruti
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imepokea fedha Tsh.Milioni 580 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 29 vya Madarasa katika shule 9 za Sekondari ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea Wanafunzi wa Kidato Cha kwanza 2023.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa