• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Sikonge District Council
Sikonge District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Idadi ya Watu
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Mifugo na uvuvi
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mazingira na Taka ngumu
      • Kilimo, Umwagilaji na Ushirika
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Uchimbaji wa Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo Ndogo
    • Miongozo Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya sanaa
      • Sanaa za picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Habari mpya
    • Matukio

SIKONGE-SERIKALI YAUPANDISHA HADHI MSITU WA ITULI

Imewekwa: June 5th, 2019

SIKONGE-SERIKALI YAUPANDISHA HADHI MSITU WA ITULU HILL

NA Evelina Odemba

SERIKALI yaupandisha hadhi Msitu wa  Itulu Hill kuwa Msitu Asilia,ikiwa ni miongoni mwa Misitu michache ya asili inayopatikana Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa wakala wa misitu Tanzania (TFS) kanda  Valentine Msusa alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Kipili iliyoko wilayani Sikonge Tabora eneo ambalo msitu huo unapatikana na kuwataka kujivunia hatua hiyo kwani mbali na kuwa na manufaa makubwa kwa serikali,  jamii itanufaika pia.

Alibainisha kuwa lengo la serikali ni kuendeleza maliasili zilizopo na kuzihifadhi ili zinufaishe kizazi kilichopo na kijacho akitolea mfano  Mti jamii ya mninga ambao umekuwa kwenye hatari ya kutoweka kwa sababu ya kuvunwa sana hivyo uwepo wa msitu huo utasaidia kuuifashi.

“hatuko tayari kupoteza Tembo wetu, hatuko tayari kupoteza miti asilia, hivyo basi yeyote atakayekiuka agizo la serikali la kuhuifadhi Msitu huu, hatutomvumilia, tutabanana nae huko huko ndani kwa ndani” alisema.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Mhe. Musalika Makungu ambaye amekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira kwa kuwataka wananchi kueshimu agizo la serikali kwa kuwa walinzi wa msitu huo huku akiwataka kutoa taarifa kwa viongozi usika mara wanapoona kundi la watu wakishiriki uharibifu wa Msitu huo.

Sambamba na hayo aliwataka wananchi kuitumia fulsa hiyo kwa kusoma masomo ya utalii kwani Msitu huo unategemewa kutumika kwa shuguli za utalii na tafiti mbalimbali. Hivyo kuwa na elimu ya utalii kwa wanajamii kutawapatia ajira itakayokuza kipato chao.

Wananchi wa Kipili wakipokea maelekezo toka kwa Mkuu wa Wilaya. Mhe. Peres Magiri aliyesimama katikati.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alipokea maelekezo hayo kwa kusema kuwa akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya atahakikisha Msitu huo unalindwa vyema, na yeyote atakayekutwa akifanya shuguli yeyote ndani ya Msitu huo bila kibali atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini. Sanjari na hayo aliishukuru serikali kwa kuupandisha msitu huo hadhi na kusema ni jambo la kujivunia kwa wana Sikonge wote.

Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUKODISHA CANTEEN [MGAHAWA] MPYA KWENYE JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZAABUNI YA KUMPATA MWEKEZAJI KATIKA KIWANDA CHA KATI CHA KUCHAKATA MAZAO YA NYUKI(MARUDIO) June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA USAFI KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI June 07, 2023
  • ZABUNI YA KUTOA HUDUMA YA ULINZI June 07, 2023
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • UZINDUZI WA SHULE YA MSINGI KININGA - KATA YA IPOLE

    May 09, 2025
  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WILAYANI SIKONGE

    May 07, 2025
  • KIKAO CHA TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE WILAYANI SIKONGE

    April 29, 2025
  • WATENDAJI WA INEC WILAYANI SIKONGE WAMEKULA KIAPO CHA UADILIFU, KUJIWEKA KANDO NA VYAMA VYA SIASA.

    April 29, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Wilayani Rungwe - Mbeya.
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Zabuni
  • Matukio
  • Matangazo
  • Habari

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Mkoa wa Tabora
  • TAMISEMI
  • Urambo DC
  • UTUMISHI
  • Kaliua DC

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC

    Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora

    Simu: 0767135460

    Simu: 0767135460

    Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma zetu

Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa