Sikonge_Tabora
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 Kwa kipindi cha Mwezi Julai-Desemba, 2022 amesema ,
Katika kuimarisha Sekta ya Kilimo Wilaya ya Sikonge, Serikali ya Awamu ya Sita imetoa Ruzuku ya Mbolea ya kupandia na kukuzia na kupunguza makali ya Bei Kwa wakulima ambapo jumla ya Tani 130.5 zimekwisha pokelewa na kununuliwa na wakulima Kwa Bei ya kuanzia Tsh.60,000-Tsh.70,000/=Kwa Mfuko wa kilo 50 Hali ambayo inatarajia kuongeza kipato na mazao ya Chakula cha Uhakika Kwa kipindi chote cha Mwaka Mzima"
"Aidha, Wilaya ina jumla ya Hekta 1,550 zinazofaa Kwa Kilimo cha Umwagiliaji Kwa mazao ya Mpunga, Mahindi na Mbogamboga kutokana na kuwapo Kwa Skimu 3 za Umwagiliaji ambazo ni Ulyanyama, Igigwa na Uluwa.
Vilevile Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji imetenga Tsh.Bilioni 3.15 Kwa ajili ya ukarabati wa Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji ya Ulyanyama ambapo ukarabati ulianza Mwezi Novemba, 2022.
#kaziiendele
#ccmkazini
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa