RADI YAUA WATANO FAMILIA MOJA.
KILIO na majonzi vyatawala baada ya watu watano wote wa familia moja kupigwa na radi hadi kufa wakiwa wamelala kitandani.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika Kata ya Mkorye, kijiji cha Isongwa, kitongoji cha Kamsini Wilayani Sikonge Tabora. Baada ya mvua kubwa iliyonyesha majira ya saa mbili usiku wa kuamkia siku ya jumanne na kuchukua uhai wa wanafamilia watano akiwemo mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Igalula.
Akiwataja marehemu hao kuwa ni Mindi Juma (ke) 40 ambaye alikuwa ni mama wa familia, Vai Juma(ke) 16, Grace Juma (ke) 13, Kulwa Lukanya (ke) 12 ambaye ndio mwanafunzi wa darasa la pili na Sia Juma (ke) 7 kaka wa marehemu Machia Petro alisema kuwa walipokea taharifa za msiba saa mbili asubuhi baada ya watoto waliosalimika kufika nyumbani na kueleza kuwa wanawaamsha wanafamilia hao na hawaamki ndipo walipochukua hatua ya kwenda kuangalia kilichojili na walipofika wakagundua kuwa watu hao walishafariki tokea usiku.
Akithibitisha vifo vilivyotokea Daktari Methew Sipemba alisema kuwa “ni kweli vifo hivi vimetokana na radi na hivyo jamii isijiingize kwenye swala la ushirikina” aliongeza kuwa tukio la radi huwa linasababisha kifo endapo muhusika atapigwa na radi kuanzia eneo la kifuani kupanda hadi juu kwakuwa mtu huvuta hewa yenye moto mkali ambayo huunguza viungo vyote vilivyo ndani ya mwili wake. Lakini ikipa eneo la miguu mtu hupata mshtuko na majeraha ya kawaida tu.
Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri akiwapa pole Wanakijiji eneo la tukio.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila alifika eneo la tukio ili kujionea na pia kutoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba huo huku akiihasa jamii kutoshiriki imani za kishirikina kwenye tukio hilo kwa kuzani kuwa ni mkono wa mtu bali waomboleze kwa amani na kuhifadhi miili ya marehemu huku wakimtanguliza Mungu katika kila jambo. Aliongeza kuwa kwa niaba ya Serikali wamesikitishwa sana na tukio lililotokea na wanaungana na wafiwa kuomboleza katika kipindi hiki kizito cha majonzi.
Katika tukio hilo pia walionusulika watoto watatu ambao ni Doto Lukanya (ke) 12, Pendo Machia (ke) 12 na Masanja Juma (me) 11 ambao walikuwa wamelala chini muda wa tukio pia walipata majeraha madogo madogo eneo la miguuni ambapo Dkt Sipemba alishauri wapewe dawa za kupinguza maumivu tu na kutoa neno kuwa majeraha hayo hayana madhara.
IMEANDALIWA NA
KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO(TEHAMA)
SIKONGE.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa