Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Cornel Magembe amesisitiza suala la kupeleka watoto shule ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wenyewe pamoja na taifa kwa ujumla,kwani kwa kusomesha watoto hapo ndipo tunavuna wataalam katika nyanja mbalimbali hivyo kusaidia taifa kuendelea kwa haraka.
Mhe. Magembe ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi katika kijiji cha Kikungu kata ya Chabutwa alipokuwa akijibu kero zilizowasilishwa na wananchi wa kijiji hicho.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe akijibu swali kuhusu bei itakayonunuliwa asali katika kiwanda cha kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki Sikonge Ndg. Pandawe amesema asali ya wafugaji wa nyuki wilaya ya Sikonge itanunuliwa kwa mfumo wa mpya wa stakabadhi ghalani utakaowezesha upatikanaji wa bei nzuri kwa wafugaji kwani mfumo huu ni kati ya mkakati wa serikali kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya nyuki na kuwainua wakulima kiuchumi nchini.
Mhe. Magembe ametoa wito kwa wananchi wa Kikungu kuchangamkia fursa kwa kuchangia shuguli za maendeleo kwani Serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa ya kuwaletea karibu huduma nyingi za msingi hivyo basi ni vema wananchi kuanzisha hata ujenzi wa boma pale wanapoona uhitaji wa huduma kama za afya unahitajika kwa haraka ili basi serikali ione juhudi zao na kuharakisha ukamilishaji wa miradi hiyo katika maeneo yao kwa wakati.
Akifunga mkutano huo diwani wa kata ya Chabutwa Mhe.Edward Peter Almasi amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Sikonge kwa kufika katika kijiji cha Kikungu na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi ,Mhe . Almasi ameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi kusukuma gurudumu la maendeleo na kumuomba DC Magembe kurudi tena wakati mwingine kuja kuzungumza na wananchi kwani kata yake ni kubwa na wananchi bado wanashauku ya kuonana na kuongea na kiongozi wao wa wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa