NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ASISITIZA UBUNIFU KATIKA VYUO VYA FDC.
SIKONGE_
28.6.2022
Naibu katiku Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia Prof. Carolyne Nombo amefanya ziara katika Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Sikonge na kukagua maendeleo ya chuo hicho na kuwasisitiza kubuni mbinu za kiubunifu ikiwemo kuanzisha miradi ambayo itasaidia chuo kujipatia kipato.
"Tufanye kwa umahili na utaalamu wa hali ya juu,ili jamii inayotuzunguka iweze kuvutiwa na kujifunza kutoka kwetu" Prof.Nombo
Aidha, Prof Nombo amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Seleman Pandawe kusimamia na kuhakikisha wananchi wananufaika kwa kupata ujuzi utakaoisaidia jamii katika mambo mbalimbali ya kiuchumi .
Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo hicho Enock Lalida amesema wananchi wameendelea kunufaika na chuo hicho ambacho kimekuwa na Mchango Mkubwa katika kutoa Ujuzi wa aina Mbalimbali kwa jamii ikiwemo TEHAMA, Umeme wa majumbani, Udereva, Ususi, Elimu Haina Mwisho, Uashi ambao sasa jamii ya Sikonge na maeneo mengine wanapata huduma zitokanazo na ujuzi huo.
Na.Anna Kapama
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa