SIKONGE- KAYA ZAIDI YA 195 ZANUFAIKA NA UMEME WA JUA ULIOZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU 2019
Na Richard Mrusha na Evelina Odemba
WANANCHI wa Kijiji cha Mgambo kilichopo Kata kitunda Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora wamesema kuwa kupata umeme kumeongeza fursa ya ajira katika kijiji hicho.
Umeme huo umetekelezwa na kampuni ya Power Corner kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliogharimu zaidi ya bilioni moja umeunganisha kaya zaidi ya 195 zilizopo katani hapo.
Akitoa taarifa wakati wa Ufunguzi wa mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Mhe. Peres Magiri alisema kuwa hivi sasa Kata ya Kitunda inafurahia huduma hiyo ya umeme wa jua na kwani umewezesha vijana kujiajiri kwa kujishughulisha na mambo mbalimbali ya uzalishaji ili waweze kujiinua kiuchumi.
Naye kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Ali wakati wa kuzindua mradi huo unaotumia umeme wa jua aliwataka wazalishaji hao kufuata bei elekezi kwa wateja wao ili wananchi wote wanufaike na mradi huo, aliongeza kuwa mpango wa Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inapeleka Umeme ndani ya Vijiji vyote ili wananchi waweze kufungua viwanda vidogo vidogo kwani nchi inaendeshwa kwa sera ya viwanda.
Akizungumza kwaniaba ya Wananchi wenzake Muuzaji wa Maji na Soda, alisema wanaipongeza sana Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Power Corner ambao ndio watekelezaji wa mradi kwani hivi sasa wanakunywa maji baridi, nyama safi ambazo zinahifadhiwa kwenye friji, ukilinganisha na awali.
Pia alisema mradi huo wameupokea kwa mikono miwili na kwakweli hawakutegemea kulingana na historia yake kwani awali walikuwa wanatumia umeme wa sola ya kawaida za kufunga wenyewe ambao pia ulikuwa hauna nguvu kama ulivyo huo uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Mkongea Ali akizindua Umeme wa Jua Power Corner ulioko kata ya kitunda Wilayani Sikonge.
"Nataka niwaeleze ndugu waandishi wa Habari leo vijana wetu wanatengeneza Simu hapahapa pindi zinapoharibika,wachomeleaji wamerahisishiwa,saluni zinafunguliwa kwakweli mambo mazuri sana." Alisema Anthon Lukas.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sikonge Martha Luleka alisema kuwa ujio wa Umeme katani hapo umeongeza chachu kwa wananchi kuweza kufanya kazi lakini pia umeimarisha usalama katika makazi ya watu ukilinganisha na huko nyuma.
Akizungumza kwa niaba ya Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila alisema kuwa Wananchi wa Kata ya Kitunda wameitumia vyema fursa hiyo kujiwezesha kiuchumi jambo linalosaidia kuongeza mapato katika Halmashauri yake. “Kipindi cha nyuma walikuwa wanafunga safari Mpaka Sikonge mjini kilomita nyingi kutoka hapa, kwa ajili ya huduma za kuchomelea n.k lakini leo hii shughuli hizi zinafanyika hapahapa kijijini kwao, ni jambo la kushukuru” alisema.
Naye Meneja Mradi Kanda ya Tabora Kutoka Kampuni hiyo ya Power Corner Erick Moshi akizungumzia mradi huo alisema Kampuni imepata ushirikiano mkubwa Kutoka mamlaka za Serikali katika kung'amua vijiji stahiki vya kupata huduma ya umeme.
Alisema kuwa mradi huo uliazishwa rasmi mwanzoni mwa mwezi Machi 2018 ambao unauwezo wa kuzalisha kilo-whatts 20 kwa kijiji cha Mgambo na umeme wenye uwezo kilo-whatts 28 kwa vijini vya Mkola na Mwenge.
Kwaupande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Mzee Ali akizungumzia mradi, kwanza alipongeza Serikali kwa kuweka Mazingira wezeshi kwa Kampuni ya Power Corner na kufikia hatua ya kuwapatia umeme wananchi.
"Nawaomba ndugu zangu wa Kijiji hiki cha Mgambo muweze kuulinda mradi huu ambao naamini umeleta fursa kubwa kwenu katika kuongeza uzalishaji Mali na kujiongezea kipato." Alisema Ali.
Alisema kuwa mradi ni mzuri na kwakuwa ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wake na Fedha ilitotumika hivyo ameuzindua rasmi kupitia Mwenge wa Uhuru 2019.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
|
|
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa