Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Leo imefanya maandamano ya amani kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri ambapo aliagiza kila Wilaya kufanya maandamano hayo siku ya tarehe 2 Julai ili kukemea na kulaani vitendo vya utoro wa wanafunzi na mimba za utotoni.
Maandamano hayo ambayo yamefanyika katika kila Kata kwa wanafunzi pamoja na wananchi kufanya maandamano kuelekea ofisi ya Kata ambapo Viongozi wa Kata wakiongozwa na Waheshimiwa Madiwani walihutubia na kukemea vitendo hivyo vya kuwakatisha masomo wanafunzi hasa wakike.
Katika Kata ya Sikonge na Misheni ziliungana kwa pamoja na kufanya maandamano yaliyojumuisha wanafunzi wa shule za msingi na za sekondari pamoja na watumishi. Maandamano hayo yalioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri kuelekea ofisini kwake ambapo alihutubia na kukemea vikali mambo yanayosababisha kwa namna moja au nyingine kukwamisha masomo ya mwanafunzi. " Hatutokuacha hivi hivi wewe utakae bainika kusababiaha mimba kwa mwanafunzi..." alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha, maafisa elimu Kata walikabidhi orodha ya wanafunzi watoro kwa Watendaji wa Kata ili kufuatilia wazazi wa hao wanafunzi na ikiwezekana kuwachukulia hatua ikiwemo faini kwa watoro sugu. Mkuu wa Wilaya aliwataka viongozi wote kuanzia ngazi ya kitongoji hadi Wilaya kushirikiana kwa pamoja ili kulimaliza tatizo hili katika Wilaya yetu na Mkoa kwa ujumla.
Kauli mbiu: Oparesheni Kamata Weka Ndani kwa Kutotii Amri halali
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa