Na.Anna Kapama_Sikonge
Baraza la Madiwani Wilaya ya Sikonge limefanya uchaguzi wa Viongozi mbalimbali wa Kamati za Kudumu na wajumbe wa Kamati hizo pamoja na nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo Mhe.Mayeka T. Mbusa Diwani wa Kata ya Kilumbi ameibuka mshindi kwa kura zote 27 kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge akitetea kiti hicho.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Seleman Pandawe amewapongeza Viongozi na wajumbe waliochaguliwa na kuahidi kutoa Ushirikiano kwao.
"Mmeonesha ukomavu katika uchaguzi, mmechagua Viongozi kwa amani, Kuna jambo nimejifunza kwenu namna ambavyo tunatakiwa kuamiana katika kupeana Uongozi, niwakaribishe katika Mwaka mwingine ,wataalamu tuko tayari kuwapa Ushirikiano katika kutekeleza shughuli za Maendeleo ya Halmashauri."DED Pandawe.
Aidha,Baraza la Madiwani limechagua wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Halmashauri ambazo ni Kamati ya Fedha na Mipango,Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Maadili ya Madiwa pamoja na Kamati ya Kudhibiti UKIMWI watakaodumu kwa Mwaka 2022/2023.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa