Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha amewataka wajumbe kushiriki ipasavyo na kuchangia Mawazo ili kupata matokeo Chanya ya lishe katika jamii ya watu wa Sikonge.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe amewasihi watendaji wa serikali kuhakikisha wanasimamia miongozo ya serikali juu ya masuala ya lishe ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa klabu za lishe mashuleni pamoja na kuweka mkazo katika usimamizi wa masuala ya lishe mashuleni hasa kupitia Uwawa (Umoja wa Wazazi na Walimu),kwani umoja huu utasaidia sana katika uratibu wa masuala ya lishe mashuleni pamoja na mambo mengine ambayo jamii inapaswa kushirikishwa moja kwa moja.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge Ndg. Andrea Ngh’wani amesema mara nyingi wataalam wanapanga vizuri lakini utekelezaji unakuwa dhaifu hivyo amemuomba Mkurugenzi jitihada zifanyike ili fedha za kutosha zipatikane na kutekeleza yale yote yaliyokusudiwa katika bajeti.
Nao wataalam wamewasilisha makadirio ya bajeti za lishe toka divisheni na vitengo mbalimbali kama ifuatavyo;Divisheni ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe imewasilisha makadirio ya bajeti ya lishe Tsh.64,932,000/=,Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Tsh.1,000,000/=,Elimu Sekondari Tsh,15,000,000/=,Maendeleo ya Jamii Tsh, 18,425,000/= na Divisheni ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Tsh,10,700,000/=.
Akihitimisha kikao hicho Mhe. Chacha amewasihi wajumbe kuzingatia yale yote yaliyochangiwa kama ushauri na mapendekezo hasa tunapoelekea katika vikao vya bajeti za mwaka lakini pia amesisitiza kulifanyia kazi agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian la kupanda miti ya Matunda katika maeneo yote kama ilivyoelekezwa hususani katika Barabara ya bomani kuelekea Ofisi za Halmashauri na Barabara ya kuelekea makazi ya Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa