Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope ameongoza baraza la waheshimiwa madiwani la siku ya kwanza la kupokea taarifa za maendeleo ya kata.
Akifungua baraza hilo Mhe. Magope amesema mbali na baraza hilo kupokea taarifa za maendeleo ya kata lakini pia litapokea taarifa za miradi mbalimbali inayotekelezwa kutoka taasisi mbalimbali za umma zinazohudumu katika halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Baraza hilo limepokea taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kitaasisi kutoka Shirika la Umeme Tanesco,TARURA,RUWASA pamoja na TUWASA.
Wakijadili taarifa za maendeleo ya kata waheshimiwa madiwani wamepongeza ukusanyaji wa mapato kutoka kata ishirini zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Sikonge uliofikia asilimia 87.1 kwa ujumla na kusisitiza mkazo uongezwe kwa kila kata kufikia malengo kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe amewashauri watendaji kuwatambua wakulima katika maeneo yao ili kuweza kufichua wafanyabiashara wanao safirisha mazao kwa kukwepa kulipa kodi kwa kisingizio kuwa wao ni wakulima tu wanaotoa mazao yao shambani na kuyapeleka majumbani mwao,hii itasadia kuzuia ukwepaji wa kodi katika maeneo mengi ya vijijini.
Akifunga baraza hilo Mhe. Magope ameipongeza timu ya ufuatiliaji wa ukusanyaji mapato kwa kutekeleza wajibu wao vizuri mbali na changamoto walizokutana nazo ikiwa ni pamoja na muda kuwa mchache na umbali kutoka eneo moja hadi jingine.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa