MAZINGE KUWA YA MFANO
KITUO cha Afya cha Mazinge kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge chatakiwa kuwa cha mfano kuhusu swala zima la usafi.
Agizo hili lilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bi. Martha Luleka alipotembelea kituo cha Afya cha Mazinge ili kuona namna wanavyoweza kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya Dengue ambao umekuwa tishio pia alikagua namna huduma za Afya zinazotolewa kituoni hapo.
Akihoji swala la usafi Bi. Martha alisikitishwa na hali aliyoikuta Mazinge ambapo baadhi ya wagonjwa walilazwa katika vitanda ambavyo havikuwa vimetandikwa mashuka ambapo Osca Magunga ambaye ni mganga kituoni hapo alijibu kuwa kumekuwa na uhaba wa maji jambo linalochelewesha kufua mashuka kwa wakati huku akihaidi kuwa tayari wanashugulikia swala hilo.
Huku akiitolea mfano Zahanati ya Kipili aliwataka watumishi wote walioko kituo cha Mazinge kujifunza usafi kupitia Zahanati ya Kipili kwa kutumia pesa za miradi mbali mbali ya Afya ikiwemo RBF kukiboresha Kituo hiko wakati akisisitiza usafi ni jukumu la kila mtu aliyepo eneo hilo hivyo basi watumishgi wote walihaswa kushiriki usafi ambapo Mganga Mkuu aliahidi kulisimamia jambo hilo.
Akizungumzia swala la utoaji wa Huduma za Afya Bi. Martha alisisitiza watoa huduma wote kujituma kwa moyo huku akiimiza kuwa serikali inatoa pesa nyingi hivy itakuwa jambo la kushangaza ikiwa wagonjwa watakosa huduma ya dawa kwani hivi sasa kumeandaliwa mpango mzuri wa kununua dawa mapema kabla ya zilizopo kuisha. Sanjari na kusema kuwa Mazinge imekuwa na wahudumu wa Afya wengi kuliko sehemu nyingine ndani ya Halmashauri ya Sikonge hivyo wajikite katika kutoa huduma bora.
Mkurugenzi Akikagua jengo la mama na mtoto katika Kituo cha Afya Mazinge
Katika ziara yake Mkurugenzi alifanikiwa kukagua Jengo la Mama na mtoto, wodi ya Wanamme na sehemu ya kufulia ambapo ilibainika kwa mashine kuwa mbovu huku Bwana Oska akitolea maelezo kuwa ufuatiliaji wa matengenezo unaendelea na mashine zitaanza kutumika wakati wowote.
Kume kuwa na wimbi kubwa la watumishi walioko Wilayani Sikonge kutibiwa katika Hospitali ya Misheni ambayo ina ubia na Serikali na sio kituo cha Mazinge ambacho ni cha serikali, jambo lililomlazimu Mkurugenzi kufanya ziara ya kushitukiza kituoni hapo ambapo alibaini changamoto hizo na tayari zinatatuliwa hivyo huduma itaendelea kupatikana kwa ubora na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA) SIKONGE
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa