"MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AMETOA FEDHA NYINGI ZA MIRADI YA MAENDELEO SIKONGE" NDG.KIHONGOSI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndg.Kenani Kihongosi ametembelea Shina la CCM namba mbili katika kijiji cha Makazi Wilayani Sikonge na kuzungumza na wananchi ikiwa ni ziara ya wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa Mkoani Tabora.
"Tumekuja kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi..lengo la serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo"Ndg.Kihongosi amefafanua.
Sambamba na hilo Ndg.Kihongosi amewataka wananchi kuungana na Viongozi ili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ufanyike kwa urahisi, huku akiwaasa baadhi ya watu wanaokwamisha shughuli hizo kwa manufaa yao binafsi kuchukuliwa hatua maramoja.Aidha,wananchi wa kijiji cha Makazi wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha za UVIKO-19 Tsh.Milioni 60 Kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba viwili vya Madarasa na ofisi moja Shule ya Sekondari Ugunda.
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imepokea Tsh.Bilioni 3.3 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Sekta ya Afya na Elimu ikiwa ni fedha za UVIKO-19.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa