Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 Kwa kipindi cha Mwezi Julai-Desemba, 2022 amesema ,
Wilaya ya Sikonge imeendelea kutekeleza agizo la Serikali la Kisheria la kutenga 10% ya makusanyo ya Mapato ya Ndani Kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na Riba Kwa makundi ya wanawake 4%, Vijana 4% na Watu wenye ulemavu 2% lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi hao kushiriki katika Shughuli za kiuchumi na kupata kipato ili kuendesha maisha yao ya kila Siku.
Aidha, katika kipindi cha Mwezi Julai-Desema 2022 Jumla ya TSH.Milioni 212 ambazo ni 10% ya Makusanyo zimepangwa kutolewa Kwa Makundi lengwa ya Mikopo hiyo baada ya Mwongozo Mpya wa utoaji Mikopo kupitia kujisajili kwenye Mfumo.
#kaziiendelee
#ccmkazini
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa