Na Linah Rwambali - Sikonge DC
Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Aldo Mwapinga amewataka Maafisa mifugo kuwajibika kwa nafasi zao ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa vishikwambi 10 kwa Maafisa mifugo Sikonge Mwapinga amesema kila mtu atakapowajibika katika eneo lake, mambo yataenda sawa.
“Tendeni majukumu yenu inavyostahili, hakikisheni mnafuata utaratibu wa ukaguzi wa nyama kama inavyoelekezwa kwa mfano mnatakiwa kufahamu nani anachinja, ng’ombe gani anachinjwa ili walaji wapate bidhaa salama”
Aidha amewataka Maafisa mifugo kuvitunza vifaa hivo walivyokabidhiwa kwakuwa ni mali ya Serikali ambayo imekabidhiwa kwao.
Naye Daktari wa Mifugo Sikonge Ndg. Maulid Mohamed amesema wametoa vishikwambi hivyo kwa Maafisa mifugo ili kuwezesha utendaji kazi wa kisasa.
“Tunawapa vifaa hivi ili kuwezesha zoezi la utoaji chanjo kwa mifugo” amesema.
Afisa Mifugo Kata ya Misheni Ndg Geofrey Matimya anasema anashukuru kwa ushauri, vifaa walivyopewa na yote waliyoshauriwa watayafanyia kazi.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa