MADIWANI WANENA.
Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora yakusanya Tsh. Bilioni 1.28 sawa na asilimia 60.7% za mapato yote yaliyokusanywa katika kipindi cha robo ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Takwimu hizi zilitolewa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mh. Peter Nzalalila katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa FDC. Wakijadili maendeleo ya Halmashauri ya Sikonge Nzalalila alihasa kuongeza juhudi kukusanya mapato ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa Sikonge.
Aliongeza kuwa mapato yanayokusanywa kwa kutumia mashine za kielectronia (POSS) yafanyike kwa uhaminifu mkubwa kwani hakutakuwa na msamaha wa aina yeyote kwa mtu atakayesababisha upotevu wa pesa na matumizi ya pesa za umma bila kupata kibali mahalumu.
Akitaja jumla ya kiasi cha sh. Ml 400 zilitolewa na Halmashauri yake kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ikiwamo Shule za msingi na sekondari ili kuboresha sekta ya Elimu.
Aidha Nzalalila alitoa wito kwa watumishi wote kuwajibika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani Serikali ya awamu hii haitomvumilia mfanyakazi yeyote asiyejituma kwani ilani ya chamam cha mapainduzi ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapatiwa huduma bora na kwa wakati sahihi ndio maana hata swala la elimu katika shule za serikali za msingi na sekondari ni bure.
Wheshimiwamadiwani wakifatilia kwa makini kikako kinachoendele.
Sanjari na hayo pia alimpongeza mkurugenzi mtendaji wa Halmashali Bi. Martha Luleka kwa mbinu alizozitumia kuhakikisha nidhamu ya kazi kwa watumishi inarejea. Akizipokea pongezi hizo Bi. Martha pia aliwahasa wakulima wasilime kwa mazoea na kulalamikia mtaji huku akitolea mfano wa wahitimu wa chuo kikuu cha SUA ambao wamekuwa wakijiunga katika makundi na kujikita katika kilimo chenye manufaa.
Akifafanua zaidi alisema mtaji ni jumla ya vitu vitatu ambavyo ni nguvu, muda pamoja na pesa kidogo hivyo basi wakulima wasibweteke kusubiri kuwezeshwa na serikali bali waanze wao kwanza na kuhakikisha wanalima kwa ajili ya kujinasua katika umasikini.
Wajumbe pia walikuwa na maoni mbali mbali ambapo waligusia zaidi juu juu ya kuhamasisha wananchi wao kushiriki katika shuguli za maendeleo kwani maendeleo ni ya wananchi wote. Hivyo wasisite kushiriki mara watakapokuwa wanahitajika.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa