MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU NGAZI YA WILAYA YAMEFANYIKA KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA-SIKONGE.
Viongozi mbalimbali Wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sikonge ambae pia ni Katibu Tawala(W) Ndg.Renatus Mahimbali wamewaongoza wananchi Wilaya ya Sikonge kufanya usafi wa Mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika.
Akizingumza na wananchi baada ya kufanya usafi huo,Katibu Tawala(W) Ndg. Mahimbali amesema Wilaya ya Sikonge imepiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kipindi cha miaka 60 katika nyanja zote za kiuchumi,kisiasa na kijamii kiasi cha kufanikiwa kufikia Uchumi wa kati ikiwa ni juhudi za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo endelevu.
"Hii ni juhudi kubwa sana katika maendeleo ya nchi na ni Jambo la kujivunia kwa Mtanzania"Ndg.Mahimbali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji(W) Ndg.Selemani Pandawe amewapongeza watumishi na wananchi kwa kujitokeza kushiriki usafi huo huku akisisitiza kuwa zoezi la usafi wa Mazingira linapaswa kuwa endelevu kwa wananchi wote ili kulinda Afya zao.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa