KAMATI YA SENSA YAFIKA KAMBI ZA WAVUVI KUHAMASISHA SENSA.
Sikonge_Tabora
Na.Anna Kapama
19.8.2022
Zikiwa zimebaki takribani Siku 4 tukio Muhimu la kuhesabu watu , Kamati ya Sensa Wilaya ya Sikonge ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe.John Palingo imefika katika Kambi mbalimbali za wavuvi katika Mto Koga ikihamasisha wananchi hao kuhesabiwa.
Akizungumza na Wananchi hao Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Wilaya ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo amewasisita kujitokeza kuhesabiwa ambapo karani atafika katika Kambi hizo ili kuwahesabu itakapofika Tarehe 23.8.2022 .
Aidha,wajumbe wa Kamati hiyo wametoa jumbe mbalimbali za umuhimu wa Kuhesabiwa kwa wakazi wa Sikonge wakiwemo wavuvi hao ili Serikali iweze kupanga Mipango ya Maendeleo Kwa kuzingatia Idadi iliyopo.
Kwa Upande wao wavuvi hao wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha siku itakapofika.
"Tutahakikisha siku hiyo tunakusanyana hata Mgonjwa tutamtoa nje ahesabiwe , hatuachi mtu" mmoja wa Wavuvi akisisitiza.
#jiandaekuhesabiwaagosti23
#sensakwamaendeleoyetu
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa