HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge, mkoani Tabora imegawa zaidi ya miti 1000 kwa shule za msingi zilizopo Wilayani hapo, ili kuboresha upatikanaji wa matunda na lishe kwa wanafunzi.
Akizungumza wakati wa kutoa miti hiyo, Afisa umwagiliaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Edgar Kasonga alisema kila shule imepewa miti 45 ya matunda tofauti. Miti iliyogawiwa ni miembe, michungwa,mipera na mapapai.
"Lengo la zoezi hili ni kuhakikisha matunda yanapatikana shuleni ili kuimarisha afya za watoto" alisema.
Aidha aliwaelekeza walimu namna ya kupanda miti hiyo na kuwaambia kuwa idara ya elimu na kilimo itafika kuangalia maendeleo ya miti hiyo.
"Mpande miti hii karibu na shule ili muweze kuifanyia ufatiliaji wa karibu, msichague eneo lolote tu ilimradi ni eneo la shule. Mwakani, idara ya Kilimo na Elimu tutakuja kukagua maendeleo ya miti mliyopanda" alisema.
Naye mwalimu wa Shule ya msingi Kipanga Mlimani, Petro Molgen alisema serikali imefanya jambo jema kwani itachangia watoto kuwa na afya bora sababu matunda ni muhimu kwa maendeleo ya afya.
Baadhi ya shule zilizopokea miti hiyo ni Chabutwa, Kabanga, Msuva, Ngoywa, Tutuo,Manyatwe, Usesula, Mpombwe, Jamhuri, Kipanga Mlimani.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa