DED PANDAWE AKUTANA NA WAFAWIDHI KUJADILI MIRADI YA AFYA INAYOTEKELEZWA KATIKA MAENEO YAO.
Na.Anna Kapama
Tarehe 22.6.2022
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg.Seleman Pandawe amefanya kikao na Kuzungumza na wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za Afya ili Kuzungumza nao na kutoa taarifa mbalimbali za Maendeleo ya Miradi ya Afya inayotekelezwa kwenye vituo hivyo ikiwa ni Siku kadhaa zimebaki kuelekea Mwisho wa Mwaka wa Fedha2021/2022.
Awali Mganga Mkuu wa Wilaya Christopher Nyalu amesema lengo la kikao hicho ni kujadili Maendeleo ya Miradi inayotekelezwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya ili kupanga Mikakati ambayo itasaidia kuhakikisha fedha zilizotolewa na Serikali zinatumika ipasavyo.
Aidha, DED Pandawe amewasisitiza wazimamizi hao kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwemo kuzingatia matumizi sahihi ya fedha kwa miradi iliyokusudiwa huku akimpongeza Katibu wa Afya Hospitali ya Wilaya ya Sikonge Masoud Ally kwa kusimamia vyema Mradi wa Ujenzi wa Majengo Sita ya Hospitali ya Wilaya yenye TSH.Bilioni 1.2.
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge inaendelea kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ya Afya, Elimu, Barabara ,Maji na mingine mingi ambayo Serikali inatoa fedha nyingi kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora.
#jiandae kuhesabiwa
#shirikisensayawatunamakazi2022
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa