DC PALINGO AMETOA SIKU 30 KWA WATOTO KUONDOLEWA MGODINI KITUNDA.
Na.Anna Kapama .Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mheshimiwa John Palingo amewataka wachimbaji walio katika Mgodi wa Kitunda kuwaondoa watoto eneo la mgodi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa Balozi Dkt Batilda Buriani kuwataka viongozi hao kuchukua hatua dhidi ya watu waliokiuka sheria na taratibu za uchimbaji madini pamoja na afya kwa watoto kuanzisha kibanda kwa kutaka kukigeuza kuwa Shule ya Msingi.
DC Palingo amefafanua zaidi kuwa kuendelea kuwaweka watoto katika mazingira hatarishi kama hapo kunawanyima haki yao ya msingi kupata Elimu,lakini pia wanakiuka sheria za afya ya mtoto .
Akitoa elimu kwa wachimba madini hao Mjiolojia kutoka ofisi ya madini Tabora Ramadhani Muhode amefafanua madhara yatokanayo na kemikali mbalimbali zinazotumika kuchenjua madini hayo kuwa zina athari kwa upumuaji hasa watoto ambao hawafahamu namna ya kujilinda na pia sheria za madini haziruhusu binadamu mwenye umri chini ya miaka 18 kuwa katika eneo la mgodi."Wakubwa mnaweza kuvaa buti (gumboot), barakoa na hata kinga za mikono(gloves) kujilinda na kemikali hizo,vipi kuhusu watoto?mnaweza kuwavalisha hata barakoa?" .Ramadhan amefafanua
Kwa upande wake Afisa Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule (W) Sikonge Sidda Nassania ametoa Elimu kuhusu utaratibu wa kuanzisha shule akitaja baadhi ya taratibu ni mazingira ya kuanzisha shule yanapaswa kuwa salama,eneo kubwa, pia mchakato unapaswa kuanzia ngazi ya kijiji,Kata na Halmashauri hivyo kwa kuanzisha shule eneo hilo halikidhi vigezo.
Mkuu wa Wilaya ameambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Rashid Magope,Kaimu Mkurugenzi Hashim Kazoka na viongozi wengine mbalimbali ambao wameahidi kuendelea kusimamia maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa