Na, Edigar Nkilabo
Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ALAT Mkoa wa Tabora wamefanya ziara katika wilaya ya Sikonge na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata za Sikonge na Tutuo ikiwemo mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Usupilo, shule ya msingi Dkt.Batilda pamoja na shule ya sekondari ya Amali ya mkoa inayogharimu shilingi bilioni 1.6 kupitia program ya kuboresha elimu ya sekondari SEQUIP.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa ALAT Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mhe. Adam Malunkwi ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Sikonge kwa kusimamia vizuri fedha zinazotolewa na serikali kuu kwa ajili ya miradi ya elimu na afya pamoja na fedha za mapato ya ndani zinazoelekezwa katika ujenzi wa ofisi za kata.
“ALAT tunakabidhi milioni 2 kwa halmashauri ya wilaya ya Sikonge kuunga mkono juhudi zao za kutenga mapato ya ndani kwa ajili ya miradi mbalimbali hasa ujenzi wa ofisi ya Kata Tutuo,huu ni mfano wa kuigwa fedha hii ikasaidie kukamisha ujenzi”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe.Rashid Magope ameishukuru ALAT mkoa wa Tabora kwa kuunga juhudi za maendeleo kwa mali na hata kutoa ushauri kwa wataalamu na wasimamizi wa miradi inayotekelezwa wilayani Sikonge.
Baadhi ya Wajumbe wa ALAT mkoa wa Tabora wameipongeza halmashauri ya wilaya ya Sikonge kwa kusimamia vizuri miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa kwa viwango stahiki vya wataalamu wa ujenzi na kuakisi thamani ya fedha.
Ziara ya ALAT mkoa wa Tabora imejumuisha wataalamu wa Idara na vitengo mbalimbali kutoka Halmashauri zote za mkoa wa Tabora.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa