Ziara ya RAS wilayani sikonge
Katibu Tawara wa Mkoa wa Tabora Mhe. Musalika Makungu afanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na vituo vya afya vilivyo katika Halmashauri ya wilaya ya sikonge mkoani Tabora.
Katika ziara hiyo pia aliambatana na wataalamu mbalimbali kutoka mkoani na wilayani sikonge. Ambao walikuwa wakitoa mawazo na kubaini changamoto zilizotokea katika ujenzi wa miradi hiyo huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge akiwa mwenyeji wa ziara hiyo.
Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ni pamoja na shule ya sekondari Pangale na kipili, Usunga,vituo vya Afya vya kitunda na kipili pamoja na mnada wa ng’ombe Mpombwe. Ambapo aliridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo na kuwataka kumalizia sehemu zilizobakia ili wakabidhi tayari kwa matumizi.
Ukaguzi ukiendelea kituo cha Afya Kitunda.
Aidha alipata nafasi ya kutembelea zahanati ya kipili na kustahajabu kwa usafi na utoaji wa huduma unaofanywa na wataalamu wa Afya hao na kuwataka kuendelea vivyo hivyo ili na wengine kote nchini waige mfano wao.
Alisisitiza swala la usafi wa mazingira ikiwemo nyumba kuwa na choo bora jambo litakalosaidia kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na kutia mkazo kwenye elimu huku akitolea mfano kuwa familia yenye wasomi huwa inamabadiliko ya kimaendeleo tofauti na familia zingine. Hivyo wazazi wawapeleke watoto wao shule na washiriki kuchangia ujenzi wa madarasa ili watoto waliokosa nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari kutokana na uhaba wa maadarasa waweze kupata mahali pa kusomea.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Sikonge pia alitoa shukrani kwa ugeni huo na kuhaidi kuyatendea kazi yale yote yalioagizwa na kuomba muda wa wiki mbili ili kukabidhi miradi hiyo. Ambapo alikaa na wataalamu wake na watendaji wa kata kujadili namna watakavyokabiliana na muda uliotolewa ili kukamilisha kazi iliyobakia na kuikabidhi.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa