Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda akiwa ziara Wilayani Sikonge amezungumza na wananchi katika viwanja vya TASAF siku ya Jumamosi tarehe 3/11/2017 na kuwataka wakulima kufikiria kulima zao mbadala la biashara kama alizeti ambayo inakipato kizuri kwa sasa na haina mgogoro katika uzalishaji.
Aidha, amesema zao la tumbaku limekuwa na mgogoro mkubwa sana kwa sasa hali ambayo inaweza kusababisha zao hili kupoteza umaarufu wake. Hata hivyo ameendelea kuiomba Wizara ya Kilimo kuharakisha mazungumzo yao na makampuni yanayonunua tumbaku ili kufikia muafaka wa kununua tumbaku ambayo bado haijanunuliwa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa