Na Linah Rwambali
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bara Steven Wasira ametoa wito kwa wananchi wote kulinda na kutunza amani ya Tanzania kwani serikali imejipanga kushughulikia watu wote watakaojaribu kusababisha ghasia kwa namna yoyote ile.
Wasira aliyasema hayo katika mkutano uliohudhuriwa na wananchi pamoja na watumishi wa serikali katika Wilaya ya Sikonge, mkoani Tabora.
“Mtu akijitokeza kutaka kuvuruga amani hatutamfumbia macho kwani kama chama tunayo dhamana ya kulinda amani ya taifa na wale wasio na sauti” alisema
“Mnapoona jambo haliko sawa acheni tabia ya kujichukulia hatua mkononi kwani vurugu ikianzishwa huathiri watu wote hata ambao hawajajihusisha katika vurugu hizo kama kina mama na watoto. Hivyo basi mnapoona kuna jambo hulielewi fateni utaratibu sahihi wa kudai haki zenu kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Sikonge Anna Chambala alimshukuru Makamu kwa kutembelea Wilaya ya Sikonge na kumuahidi kuwa yale yote aliyozungumza katika mkutano huo watayafanyia kazi.
“Tunashukuru kwa kutembelea na tunaahidi kutekeleza yale yote uliyotuelekeza katika mkutano huu wa leo” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa