ZAIDI YA SH.MILIONI 20 ZATOLEWA KUJENGA MADARASA,OFISI ZA WALIMU NA VYOO SHULE YA MSINGI KILOLELI-"RWAMBANO CUP".
Mbuge jimbo la Sikonge,Mhe.Joseph Kakunda amechangia Sh.M 10.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,ofisi za walimu pamoja vyoo shule ya Msingi Kiloleli alipokaribishwa akiwa Mgeni rasmi katika fainali ya mashindano ya mpira wa miguu maarufu kwa jina la "RWAMBANO CUP".
Mashindano hayo yalianzishwa na diwani kata ya Kiloleli Mhe.Gasto Rwambano kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, vyoo pamoja na ofisi za walimu shule ya Msingi Kiloleli.
Mhe.Rwambano amefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh.Milioni 9 zilizotokana na kiingilio kutoka kwa wananchi waliohudhuria katika mashindano hayo tangu yalipoanzishwa.
Aidha,Mhe.Kakunda amempongeza Mhe.Rwambano kwa kuwa mbunifu katika kuleta maendeleo kata ya Kiloleli,huku akiwaasa Madiwani kata zingine kuiga mfano huo ili kuhamasisha maendeleo kwa wananchi wa Sikonge.
Fainali hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya Mhe.John Palingo ambae pia amechangia Tsh.Laki moja, huku waheshimiwa madiwani kwa pamoja wakichangia zaidi ya Sh.laki mbili,na Viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Mwenyekiti Mhe.Anna Chambala.
Katika fainali hiyo iliyohusisha timu ya "Tumbaku FC" kutoka kata ya Kipanga imeibuka kidedea kwa kushinda gori moja(1) kwa nunge(0) dhidi ya "Kiloleli FC"ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa