WILAYA YA SIKONGE YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI.
Na.Anna Kapama
Tarehe 5.6.2022
Ikiwa ni Siku ya Mazingira Duniani Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imeadhimisha siku hiyo kwa kupanda Miti katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kata ya Pangale, ambapo Viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Sikonge Faraja Hebel, Wakala wa Misitu(TFS) Wilaya ya Sikonge, na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi.
Kaimu Katibu Tawala Faraja Hebel amewasisitiza wananchi kutunza Mazingira kwa kupanda Miti pamoja na kutunza vyanzo vya Maji kwa kuwa ni muhimu kwa maisha ya wanadamu na viumbe hai.
Aidha, Hebel amewaasa wananchi kutokufanya Shughuli za kibinadamu kwenye Vyanzo vya Maji akiwataka kuwa mabalozi wazuri katika kutunza vyanzo hivyo kwa kupanda Miti.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Mazingira Wilaya ya Sikonge Bwenge Mwesigwa ametoa Elimu ya upandaji Miti na namna ya kuitunza na kuongeza kuwa upandaji na utunzaji wa Miti unapaswa kuwa endelevu na siyo siku maalumu.
Katika kuunga mkono juhudi za kuhifadhi Mazingira Ofisi ya Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Sikonge imetoa Miche 483 ambayo imepandwa na Viongozi pamoja na wananchi katika maeneo yao.
#Tanzania ni moja.Tunza Mazingira
#jiandaekuhesabiwa2022
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa