WAZIRI OR- TAMISEMI ATUA SIKONGE JANA
Waziri OR- TAMISEMI, Mhe. Seleman Jafo apita Sikonge kusalimia na Kutembelea mradi wa Ujenzi wa Jengo la ofisi za Halmashauri akitokea Mkoani Katavi .
Akizungumza na wakuu wa Idara, viongozi wa Chama tawala na baadhi ya wajumbe wa Kuu Wilaya katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kukaribishwa na DC Peres Magiri, ameeleza jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza Ilani ya Chama tawala CCM ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya ambavyo vitasaidia sana kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Aidha, ameagiza miradi yote ya ujenzi isimamiwe vizuri na ikamilike kwa asilimia 100, pia izingatie ramani maalum zilizoelekezwa ambazo zinapatikana katika tovuti ya TAMISEMI na kusisitiza vifaa vyote vya Ujenzi vitumike kutoka viwanda vya ndani ili kuunga mkono jitihada za Rais Mhe. Dakt. John Magufuli kuhusu serikali ya viwanda .
Pia, ametumia nafasi hii kuwapongeza wananchi Sikonge na Mbunge wa jimbo la Sikonge, Mhe. Joseph Kakunda kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Mhe. Jafo alikagua Ujenzi wa Jengo la ofisi za Halmashauri na kutoa maelekezo kuwa jengo hilo liishie orofa mbili kwa sababu ni kubwa sana ukilinganisha na majengo ya Halmashauri zingine. "Halmashauri bado inamajukumu makubwa hasa ya Miradi ya Afya na Ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wananchi" alisema Mhe.Seleman Jafo (MB). Pia Alimtaka Mkandarasi kuharakisha Ujenzi hadi kufikia Mwakani Mwezi Mei liwelimekamilika na kuanza kutumika.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA TEHAMA
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa