."WATUMISHI WA HALMASHAURI YA SIKONGE OGOPENI FEDHA ZA MAENDELEO"DHRO KAYANGE.
Ziara ya Mkurugenzi kuwatembelea watumishi Wilayani Sikonge imeendelea Leo katika kata tatu za Mpombwe, Pangale na Igigwa ambapo amekutana nao na kusikiliza kero mbalimbali ambazo wanakumbana nazo wakiwa katika kutekeleza majukumu yao huku akitoa maelekezo na maagizo mbalimbali kwa watumishi hao ili waweze kutoa huduma bora kwa jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Mkuu wa Idara ya Utawala na Raslimali watu(W) NIKO KAYANGE amesema fedha zinazotolewa na serikali ya awamu ya Sita kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinapaswa kuheshimiwa na kuelekezwa katika miradi iliyopangwa ili wananchi wanufaike na si vinginevyo huku akiwaonya watumishi wanaosimamia miradi hiyo kuepuka ubadhilifu."Watumishi mnaosimamia miradi ya maendeleo...ogopeni fedha za Serikali" DHRO Kayange.
Aidha,DHRO Kayange amewasisitiza watumishi wote wa Umma Wilayani Sikonge kushirikiana ili kutatua kero mbalimbali za wananchi huku akiwaasa kuzingatia miiko ya utumishi wa Umma.Miongoni mwa kero zilitowasiliswa na watumishi ni pamoja na uchakavu wa miundombinu ya baadhi ya majengo ya kutolea huduma katika sekta ya Elimu na Afya kero ambazo kwa sasa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kutoa fedha za kujenga na kuboresha miundombinu hiyo.
Na Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa